Rais Paul kagame wa Rwanda, amteua Francis Gatare kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Maendeleo.
Gatare amechukua nafasi ya Clare Akamanzi aliyehudumu kwa cheo hicho, kwa Zaidi ya miaka 6.
Mchumi huyo amewahi kushika nafasi mbalimbali katika serikali ya Rwanda.
Miongoni nafasi alizowahi kushika ni pamoja na Mshauri wa Uchumi wa Rais Kagame na Mtendaji wa Bodi ya Madini na nishati.
Muda mfupi baada ya kuteuliwa alisema ndoto yake ya kukuza uchumi wa Rwanda kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa X.
Mbali na uteuzi huo wa Francis Gatare, pia Rais Kagame ameteua watu kwengine watano kushika nafasi mbalimbali.
Amemteua Jenerali Mstaafu James Kabarebe kuwa waziri wa mambo ya Nje.
Dr. Yvone Umulisa ameteuliwa kuwa katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Profesa Manaseh Nshuti ameteuliwa kuwa mshauri wa Raisi katika kazi Maalumu
Bw. Alphonse Rukaburandekwe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Nyumba Rwanda (RHA).
Na mwisho amemteua Bw. Bonny Musefano kuwa mshauri katika ubalozi Rwanda uliopo Tokyo, Japan.
Bado Rais Kagame abaendelea kubadili Uongozi wa Rwanda kidogo kidogo, hii ni baada ya kufanya mabadiliko makubwa jeshini.