ZINAZOVUMA:

Jeshi lachukua madaraka nchini Niger

Wanajeshi nchini Niger wametangaza kumuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo...

Share na:

Wanajeshi nchini Niger Jana Jumatano Julai 27, 2023 wametangaza kumtoa madarakani Rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum kwa madai ya kushindwa kutawala vizuri na kushindwa kusimamia usalama.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Niger, Kanali Amodou Abramane katika kituo cha Taifa cha Runinga nchini humo cha West Africa TV.

“Tunautamatisha utawala huu, Kama mnavyojua kwasababu ya kushindwa kuwa na utawala bora na kushindwa kusimamia vizuri usalama wa nchi,” amesema Kanali Abramane akiwa amezungukwa na wanajeshi wengine.

Aidha, Abdramane amesema mipaka ya Niger imefungwa, amri ya kutotoka nje imetangazwa nchini kote, na taasisi zote za jamuhuri zimesitishwa.

Wanajeshi hao walionya dhidi ya uingiliaji kati wowote wa mataifa ya kigeni katika mapinduzi hayo.

Kuchukuliwa kwa jeshi kwa nchi hiyo yanafanya idadi ya mapinduzi kufikia saba katika eneo la Afrika Magharibi tangu mwaka 2020 jambo linalotajwa huenda likasababisha ugumu wa kupambana na ugaidi katika maeneo hayo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya