ZINAZOVUMA:

Indonesia yavuliwa nafasi ya kuwa mwenyeji kombe la dunia.

Indonesia imevuliwa nafasi ya kuwa mwenyeji katika mashindano ya kombe...

Share na:

Shirikisho la mpira Duniani FIFA limewaondoa Indonesia kama wenyeji katika michuano ya kombe la dunia la vijana chini ya miaka 20 itakayofanyika kuanzia Mei 20 mpka Juni 11 2023.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya serikali ya Indonesia kukataa kuipokea timu ya Israel kutokana na mgogoro wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo.

Indonesia ni mshirika wa Palestine hivyo kulipokea Taifa la Israel katika michuano hiyo kumeibua hisia kubwa kwa wananchi na kufanya waandamane kupinga ujio wa Israel nchini mwao.

Raisi wa FIFA Gianni Infantino amesema mwenyeji mpya wa mashindano hayo atatangazwa hivi karibuni lakini tarehe iliyopangwa awali haitobadilika.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya