Serikali ya India imewaamuru watengenezaji wa dawa za kikohozi kupima sampuli ya dawa hizo kabla ya kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
Kuanzia tarehe 1 Juni, kampuni hizo zitalazimika kupata cheti cha uchambuzi kutoka kwa maabara iliyoidhinishwa na serikali.
Mabadiliko haya ya sheria yanakuja baada ya baadhi ya dawa za kikohozi zilizotengenezwa India kuhusishwa na vifo nchini Gambia na Uzbekistan.
Mabishano hayo yalikuwa yameleta dosari katika tasnia ya dawa ya India, ambayo inafanya theluthi moja ya utengebezaji wa dawa duniani.
Tangazo hilo lilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Biashara ya Kigeni, ambaye alisema katika taarifa yake kwamba dawa za kikohozi zitaruhusiwa kusafirishwa nje ya nchi baada ya sampuli ya dawa zitakazosafirishwa nje kuchunguzwa.