ZINAZOVUMA:

Ikulu ya Chamwino yazinduliwa

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amezindua rasmi Ikulu...

Share na:

Raisi Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Ikulu ya Chamwino iliyopo jijini Dodoma leo Jumamosi Mei 20, 2023.

Raisi Samia ambaye ameongozana na viongozi mbali mbali kwenye uzinduzi huo akiwemo makamu wake, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi na viongozi wengine wengi.

Katika uzinduzi huo Raisi Samia Suluhu Hassan ameotesha mti wa kumbukumbu ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Ofisi ya Rais Ikulu Chamwino Dodoma.

Ikulu ya Chamwino ina ukubwa wa ekari 8,473 ambazo ni ongezeko kutoka ekari 66 za awali. Ikulu hiyo pia ina eneo kubwa zaidi ya mara 200 ukilinganisha na ile ya Dar es Salaam (Magogoni) ambayo inachukua eneo la ukubwa wa Ekari 41.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,