ZINAZOVUMA:

Hospitali ya Muhimbili kujenga upya

Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesema hospitali hiyo...

Share na:

Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam umesema hospitali hiyo itabomolewa na kujengwa upya.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa Muhimbili ni moja kati ya miradi saba mikubwa ya Serikali iliyoidhinishwa, hivyo itabomolewa na kuanza ujenzi upya.

“Lakini itakwenda kwa awamu si kwamba itajengwa kwa wakati mmoja. Awamu ya kwanza tutaanza upande wa makuti kisha katikati na tutaenda na mbele. Tutaona hospitali nyingine mpya ambayo itakuwa na ukubwa kama huu wa sasa lakini majengo yatakuwa ya kisasazaidi,” amesema Prof. Janabi..

Prof. Janabi amesema kuwa gharama ya kujenga upya hospitali hiyo itakuwa ni zaidi ya Sh bilioni 600 ambazo wamepatiwa kama mkopo nafuu kutoka benki ya Exim na utaanza kulipwa baada ya miaka 25.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya