ZINAZOVUMA:

Hali ya ‘Twitter’ si shwari

Mtandao wa twitter umepoteza karibu nusu ya mapato yake ya...

Share na:

Mtandao wa Twitter umepoteza karibu nusu ya mapato yake ya utangazaji tangu uliponunuliwa na Elon Musk kwa Dola bilioni 44 (£33.6bn) Oktoba mwaka jana.

Taarifa zinasema kwamba mtandao huo haujaona ongezeko la mauzo na mapato ambalo lilikuwa linatarajiwa mwezi wa sita.

Huenda hatua hiyo imechangiwa na Elon Musk kuwafuta kazi takriban nusu ya wafanyakazi 7,500 wa Twitter alipochukua wadhifa huo mwaka wa 2022 katika juhudi za kupunguza gharama.

Wakati huo huo, Twitter inajitahidi kupambana na mzigo mkubwa wa madeni huku mtiririko wa pesa ukiwa mbaya.

Elon Musk alisema mwishoni mwa wiki kwamba ingawa hakuweka wazi muda wa kushuka kwa 50% ya mapato ya matangazo, Katika tweet alisema:

“Tunahitaji kufikia mzunguko mzuri wa pesa kabla ya kuwa na anasa ya kitu kingine chochote.”

Wakati hayo yakiendelea Mpinzani wa mtandao wa twitter, Threads sasa una watumiaji milioni 150, kulingana na makadirio yaliyopo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya