Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima amewaomba wanamichezo kupitia Vilabu vyao kuungana na Serikali kupaza sauti ya kuhamasisha wananchi kudhibiti mmomonyoko wa maadili unaochochea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwa watoto.
Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito huo alipokutana na rais wa Klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said Aprili 7, 2023 jijini Dar es salaam ikiwa na mwanzo wa ziara yake ya kutembelea vilabu vya Michezo kuhamasisha kada hiyo kushiriki kampeni ya ZIFIUKUKI (Zijue Fursa, Imarisha Uchumi, Kataa Ukatili, Kazi lendelee)
Akiilezea kampeni hiyo Dkt. Gwajima amesema lengo ni kuelimisha jamii kuhusu fursa mbalimbali za uwezeshaji kiuchumi eneo ambalo wananchi wengi wanaonekana kutofahamu husuan ni wa viijijini kwakuwa mifumo ya taarifa haiwafikii.
Waziri Dkt. Gwajima amesema Ajenda ya kulinda maadili ya jamii ni Jambo mtambuka ndani ya taifa, hivyo ni muhimu sekta zote ikiwemo ya vilabu vya Mipira, na Sanaa mbalimbali kupitia majukwaa yao pamoja na mitandao ya kijamii kulikemea kwa nguvu zote.