ZINAZOVUMA:

Gari la Balozi wa Uturuki lashambuliwa Sudan

Gari la Balozi wa Uturuki nchini Sudan limeshambuliwa siku ya...

Share na:

Gari rasmi la balozi wa Uturuki nchini Sudan lilipigwa risasi siku ya Jana jumamosi wakati mapigano yakiendelea kati ya jeshi na kundi la wanamgambo katika mji mkuu wa Khartoum.

Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha milio ya risasi iliyopigwa katika gari la Balozi Ismail Cobanoglu wala kujulikana kwa kundi lililohusika na shambulizi hilo.

Hata hivyo hali nchini humo si shwali toka kuanzishwa kwa mapigano kati ya majenerali wawili, Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) Mohammed Hamdan “Hemedti” Dagalo yaliyozuka Aprili 15, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 550 na maelfu kujeruhiwa hadi sasa.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya