ZINAZOVUMA:

Fursa ya Kiswahili nje ya nchi

Balozi 13 za Tanzania nje ya nchi zimetangaza fursa ya...

Share na:

Balozi 13 za Tanzania nje ya nchi zimetenga vituo na madarasa kwa ajili ya kufundisha Kiswahili, huku pia kukiwa na mkakati wa kuongeza na vyuo mbalimbali ili kuitangaza zaidi lugha hiyo duniani.

Kufunguliwa kwa vituo hivyo, jumla ya Watanzania 95 wamepata ajira katika maeneo hayo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Ameir Abdallah Ameir aliyetaka kujua namna Balozi zinavyotumia fursa ya kukua kwa lugha ya Kiswahili nje ya nchi.

Mbali na fursa hizo, Naibu Waziri ameongeza kuwa vyuo na vituo binafsi zaidi ya 150 vinafundisha Kiswahili duniani.

“Kwa sasa, Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limepewa kazi ya kufundisha walimu kumi (10) wa Diaspora katika Ubalozi wetu wa Abu Dhabi ambao ulihitaji walimu wa kwenda kufundisha Kiswahili katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

“Baadhi ya Balozi zetu zipo katika mazungumzo na vyuo vikuu kwenye maeneo yao ya uwakilishi ili lugha ya Kiswahili iweze kujumuishwa katika mitaala ya vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na kupata wahadhiri wa Kiswahili kutoka Tanzania,”

Miongoni mwa vyuo hiyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kuwait, Chuo Kikuu cha Holon Institute of Technology nchini Israel na Chuo Kikuu cha Buraimi nchini Oman.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya