ZINAZOVUMA:

Funga (swaumu) yake yamponza.

Mchezaji akosa nafasi ya kucheza sababu ya msimamo wake wa...

Share na:

Mchezaji wa timu ya Nates Jaoune Hadjam (20) inayoshiriki “league 1” ya nchini ufarasa hakujumuishwa kwenye kikosi baada ya msimamo wake wa kutokubali kufungua (swaumu) funga yake kama alivyotaka kocha wake.

Katika mchezo uliochezwa siku ya jumapili dhidi ya “Stade de Reims” beki huyo hakupata nafasi na mechi hiyo ilimalizika kwa Nates kupoteza mchezo huo.

Kocha wa timu ya Nates, Antonie Komboure anasema anaheshimu maamuzi ya mchezaji huyo na anawaunga mkono wale wanaofunga katika timu yake lakini wakati wa mechi hawatakiwi kufunga na hiyo sio adhabu bali yeye ndio anapanga sheria za timu.

Aidha mchezaji huyo alisema atakua tayari kutofunga katika mechi za ugenini tu lakini mechi zitakazochezwa katika uwanja wa nyumbani basi ataendelea na ibada yake ya swaumu.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya