ZINAZOVUMA:

Fainali ya Yanga yabadili ratiba NBC

Ligi kuu imetangaza kusogeza mbele kucheza michezo ya mzunguko wa...

Share na:

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa taarifa kuwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 zitacheza michezo yao ya mwisho mzunguko wa 30 Juni 9, 2023 ili kutoa nafasi kwa klabu ya Young Africans kucheza michezo yake miwili ya fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Mei 28 na Juni 3, 2023 dhidi ya klabu ya USM Algiers ya nchini Algeria,

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC iliyotumwa kwa klabu hivi karibuni na kutangazwa kwa umma jana, michezo ya mwisho kwa klabu zote ukiondoa Tanzania Prisons na Young Africans ilipangwa kufanyika Mei 28, 2023 lakini Bodi imelazimika kufanya mabadiliko hayo baada ya majadiliano ya ndani yaliyojikita katika kuhakikisha uwepo wa haki na usawa michezoni kwa kuondoa mazingira yanayoweza kuchangia upangaji wa matokeo katika michezo hiyo.

Mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na mabadiliko ya tarehe ya michezo ya mzunguko wa 29 ambapo sasa timu zote zitacheza Juni 6, 2023.

Bodi inatambua kuwa klabu zilianza kufanya maandalizi ya michezo hiyo kwa tarehe zilizotangazwa awali na kwa masikitiko inafahamu kuwa mabadiliko haya yanaweza kuathiri maandalizi hayo kwa namna moja ama nyingine. Hata hivyo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa imelazimika kufanya mabadiliko hayo kwa maslahi mapana ya ligi na mpira wetu kwa ujumla.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya