ZINAZOVUMA:

ECOWAS yapeleka kikosi Niger

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeidhinisha...

Share na:

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeidhinisha hatua ya kijeshi kutumika nchini Niger dhidi ya viongozi wa kijeshi walioingia madarakani kwa kuipindua serikali ya Rais Mohamed Bazoum.

ECOWAS imesema inaweka tayari kikosi cha kijeshi kitakachofanya operesheni Niger ili kurejesha utawala unaotambulika kikatiba.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo amesema matumizi ya nguvu za kijeshi itakuwa ni njia ya mwisho ikiwa jeshi hilo halitakubali mazungumzo.

Rais wa Ivory Coast Alassane Outarra amesema takriban wanajeshi elfu moja wa nchi yake watajiunga na kikosi hicho.

Wiki iliyopita, nchi za Senegal, Benin na Ivory Coast zilijitolea kupeleka wanajeshi iwapo jumuiya hiyo ya kikanda itaamua kuingilia kijeshi nchini Niger.

Kamishna wa ECOWAS wa Masuala ya Kisiasa, Usalama na Amani, Abdel -Fatau Musah alisema kwamba wanajeshi watatumwa wakati wowote.

“Hatutafanya mazungumzo milele. Operesheni hiyo itasitishwa tu ikiwa mamlaka ya kijeshi ya Niger litaamua kufanya mazungumzo ya kumrejesha madarakani Rais Bazoum na kuirejesha nchi kwenye utawala wa kikatiba”. Alisema.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya