ZINAZOVUMA:

ECOWAS yaendelee na maandalizi kuivamia Niger

Jeshi la ECOWAS limeviweka vikosi vyake vya dharula tayari kwa...
Members of a military council that staged a coup in Niger attend a rally at a stadium in Niamey, Niger, August 6, 2023. REUTERS/Mahamadou Hamidou NO RESALES. NO ARCHIVES

Share na:

Licha ya raia wa Niger kuandamana kupinga uingiliaji kati wowote wa kijeshi wa ECOWAS nchini kwao bado jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi inaendelea na mipango ya kuingilia kati kijeshi kurejesha demokrasia na kumrejesha Raisi Mohammed Bazoum kweye nafasi yake.

Kulingana na vyanzo vya karibu bado mchakato unaendelea wa mipango hiyo ambayo iliidhinishwa mjini Accra na kwa sasa inatoa nafasi ya kutumwa kwa wanajeshi kwenda Niger.

Viongozi wa kijeshi wa kikosi cha dharura wa Jumuiya ya ECOWAS wako tayari kutuma vikosi vyao nchini Niger, huku wakisema kuwa hawajapokea amri ya kusitisha kuivamia Niger.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, wakuu wa majeshi kwa sasa wanasimamia zoezi la kupelekwa kwa wanajeshi wao. Katika awamu hii ya uanzishwaji, nchi zilizo mbali na Niger zimekubali kutuma wanajeshi wao katika nchi zinazopakana na Niger, zilizochaguliwa kama ngome.

Taarifa za hivi punde zinaonyesha kuwa kikosi cha dharura cha ECOWAS kitaundwa na wanajeshi kutoka Benin, Nigeria, Senegal, Ivory Coast Guinea-Bissau pamoja na Ghana.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya