ZINAZOVUMA:

Dkt Ashatu Kijaji: Wafanyabiashara nipigieni simu mkikwama

Waziri wa biashara Dokta Ashatu Kijaji awataka wafanyabiashara kumåpigia simu...

Share na:

Waziri wa viwanda na biashara dkt. Ashatu Kijaji amewataka wafanyabiashara kumtaarifu wanapokwama katika mlolongo wa utendaji wa serikali.

Dokta Kijaji amesema hayo katika maonyesho yaliliyoandaliwa na BRELA, ili kuhamasisha usajili wa biashara.

Amesema hivyo ili kupunguza adha kwa wafanyabiashara, hali ambayo hupelekea biashara nyingi kufungwa.

Kufunga biashra maana yake unadhoofisha uchumi. Simu yangu ipo wazi saa ishirini na nne kwa siku nipigie unaimbie nayekuja kufunga biashara yako hata usiku”.

Kauli hii kali kutoka kwa waziri imekuja baada ya malalamiko ya wafanyabiashara kuwa, kuna baadhi ya taasisi za serikali huwasumbua na kuwataka wfunge biashara pasipo kutafuta njia mbadala.

Pia Dokta Kijaji ameeleza taasisi mbalimbali zinazoshughulika na wafanyabiashara, kukaa na wahusika na kujadiliana nao badala ya kufunga biashara zao.

Na kuongeza kuwa shughuli hizo za iuchumi ndio zinatoa ajira kwa vijana na kuchangia ukuaji wa taifa.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya