Waziri wa uwekezaji, viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amekitaka kiwanda cha kutengeneza viuadudu TBPL kilichopo kibaha mkoani pwani kuhakikisha kinajitangaza ndani na nje ya nchi ili kuiongeza wigo wa masoko na kuuza bidhaa hiyo ya kipekee.
Dkt Kijaji ameyasema hayo leo alipotembelea kiwanda hicho kuona namna uzalishaji wa viuadudu unavyofanyika.
Akiwa kiwandani hapo Dkt Kijaji amekitaka kuhakikisha kinajitangaza Kwa nguvu zote ili kupata soko la nje na ndani na si kutegemea soko la ndani pekee ambalo kwa kiasi kikubwa si la kuridhisha.
Aidha Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo NDC ambalo ndio mmiliki wa kiwanda hicho Alfred Mapunda amesema wameanza utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kimasoko pamoja na kuanza mchakato wa kutafuta mawakala wa kuuza na kusambaza dawa nchini.