ZINAZOVUMA:

Tanzania kuhamia uchumi wa kidijitali

Serikali imedhamiria kuhimiza nchi kuelekea katika mfumo wa uchumi wa...

Share na:

Serikali imesema imedhamiria kuharakisha nchi kuelekea katika uchumi wa kidijitali hususani kuhimiza mfumo wa kufanya biashara bila fedha taslimu (cashless economy), ambao unaowezeshwa na kuendeshwa na TEHAMA.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma leo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24.

“Ili kufanikisha haya kwenye sekta zote za uchumi na kijamii, Wizara imepanga kufanya mabadiliko na maboresho makubwa kwenye sekta ili kuendana na mageuzi haya ikiwemo kuharakisha ujenzi, uendelezaji na usimamiaji miundombinu ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.

“Vilevile, Wizara itafanya mapinduzi kwenye Taasisi za Sekta; kuimarisha mashirikiano na Sekta binafsi, kuendeleza tafiti na ubunifu kwenye masuala ya TEHAMA ikiwemo uanzishwaji na uendelezaji wa kampuni changa (startups), kuwezesha Sekta nyingine kuelekea kwenye mapinduzi haya ya kidijitali; na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,