ZINAZOVUMA:

Dkt Ndumbaro ajiuzulu nafasi yake Tff

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro amejiuzulu...

Share na:

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt Damas Ndumbaro amejiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Katika barua yake kwa Rais wa TFF, Mheshimiwa Waziri alisema kutokana na wadhifa wake mpya inamlazimu kujiuzulu wadhifa huo.

Alisema amelazimika kujiuzulu nafasi hiyo ili atekeleze majukumu aliyopewa kwa haki na kuepusha mgongano wa maslahi.

Agosti 30 mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alimteua Dkt. Ndumbaro kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Karia amepokea uamuzi huo wa Mheshimiwa Waziri na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.


Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,