Makamu wa Raisi wa Tanzania Dkt Philip Isidory Mpango ameliagiza jeshi la polisi kutokufunga barabara kwa muda mrefu pindi msafara wa viongozi unapokuwa unapita.
Dkt Mpango ameyasema hayo leo tarehe 13 Aprili 2023 akiwa mkoani Mwanza katika ziara yake ikiwa leo ni siku ya tatu akiwa mkoani hapo.
Wakati akizungumza na wananchi Dkt Mpango amewaomba radhi wananchi kwa adha wanayoipata kwa kusimamishwa muda mrefu barabarani huku akitolea mfano barabara kufungwa kwa takribani saa nne kumsubiri apite.