ZINAZOVUMA:

Dkt. Biteko: Tumuenzi Sokoine

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati dkt. Dotto...

Share na:

Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema watanzania tumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi na maisha Yao kwa ujumla.

Ambaye aliwahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania wakati Baba wa Taifa akiwa Rais wa Tanzania.

Dkt.Boteko ameyasema hayo wakati wakati akimuwakilisha Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Mdahalo wa Kumbukizi ya Waziri Mkuu huyo wa Zamani.

Mdahalo wa kitaifa wa kumbukizi wa miaka 40 ya Edward Moringe Sokoine ulifanyika katika chuo kikuu cha SUA, mkoani Morogoro.

Waziri Biteko amesema kuwa Sokoine atakumbukwa daima kama kiongozi aliyepigania maendeleo ya taifa kwa moyo wake wote na alitilia mkazo kuwa wananchi ndiyo msingi maendeleo.

“Hayati Sokoine alifanya kazi kubwa katika shughuli mbalimbali za maendelea ya taifa na aliweka misingi imara iliyoendeleza muongozo wa kila kiongozi wa Tanzania awe wa namna gani” amesema Dkt. Biteko.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya