ZINAZOVUMA:

De gea amesema ‘ni muda wa kutafuta changamoto mpya’

Golikipa wa Manchester United David De Gea amemaliza mkataba wake...

Share na:

Kipa wa Manchester United na Uhispania David de Gea amesema ni wakati mwafaka wa yeye kwenda kutafuta changamoto mpya sehemu nyingne huku akithibitisha kuwa anaondoka Manchester United msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake katika klabu hiyo ya Old Trafford kukamilika mwishoni mwa Juni.

De Gea amekuwa mchezaji wa Manchester United kwa miaka 12 akicheza mechi 545 na akicheza mechi 190 bila kufungwa ambayo ni rekodi za juu kwa klabu akiwa kama kipa.

“Nilitaka tu kutuma ujumbe huu wa kuwaaga mashabiki wote wa Manchester United,” aliandika kwenye mtandao wa kijami wa twitter.

De Gea alianza soka lake katika klabu ya Atletico Madrid lakini alijiunga na United kwa £18.9m mwaka 2011 na toka wakati huo ameitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa sana.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,