ZINAZOVUMA:

Dar kufuta shule za kutwa za sekondari

Katika jitihada za kudhibiti maadili na kuboresha elimu ya vijana...

Share na:

Katika kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule za kutwa.

Chalamila, ameyasema hayo leo Agosti 14, 2023 katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya awamu ya Tano ya kukabidhi magari kwa Maafisa Elimu wa Sekondari kwa Halmashauri nane.

Amesema, Mkoa wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200.

Amesema, pamoja na kwamba Dar es Salaam ina shule nyingi, kidato cha sita ndio inafanya vizuri lakini kidato cha nne bado ni changamoto kwa sababu kuna shule nyingi sio za bweni.

“Na kwa sababu ya vitendo vingi vinavyoendelea mitaani ikiwemo ukosefu wa maadili, foleni, pamoja na changamoto nyingine, sisi tumeshakaa kikao chetu na shule zetu, tumepanga mipango kwamba sasa tujipe muda tuanze kufuta shule za kutwa ili hapa katikati kote tuwe na shule za bweni tu..” Amesema Chalamila na kuongeza

“Tutafuta shule za kutwa tubaki na Bweni hii itasaidia kumanage nidhamu ya wanafunzi katika makuzi yao lakini pia muda wanaofika shule na hata walimu wa ziada ni rahisi kuweza kuwamanage wanapokuwa pamoja.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya