ZINAZOVUMA:

Crimea kuuza nyumba ya Zelensky

Serikali ya eneo huru la Crimea pembezoni mwa Ukraine, limeanza...

Share na:

Serikali ya Crimea yataifisha mali za serikali na wafanyabiashara wakubwa kutoka Ukraine.

Eneo hilo ambalo lilikuwa ni sehemu ya Ukraine hadi mwaka 2014, limekuwa chini ya Urusi kwa takriban miaka 9 tangu kuchukuliwa.

Spika wa bunge la Crimea Vladimir Konstantinov alisema kuwa mali hizo zilizotaifishwa na serikali yao, zinatarajiwa kupigwa mnada hivi karibuni.

jengo linaloaminika kuwa na nyumba ya Zelensky iliyopo Crimea
Jengo linaloaminika kuwa na nyumba ya Zelensky iliyopo Crimea

Na kuongeza kuwa tayari walishauza baadhi ya mali kwa mnada, na kujipatia Zaidi ya dola milioni 8.5 za marekani sawa na Shilingi Bilioni 21 za Tanzania.

Katika mali hizo zilizotaifishwa, zipo pia mali za watu wakubwa nchini Ukraine, ikiwe moja ya Raisi Volodymyr Zelensiky wa Ukraine.

Wengi wanaamini kuwa serikali hiyo, inapata msukumo wa kuuza mali hizo kutoka Urusi.

Viwango vya kubadili fedha $1= 2500TZS

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,