ZINAZOVUMA:

Zelenskiy akasirishwa na maamuzi ya NATO

Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekasirika kwa hatua ya NATO...

Share na:

NATO haijakubali moja kwa moja kuipa ruhusu Ukraine kujiunga na umoja huo katika kikao cha kwanza kilichofanyika Jana siku ya jumanne.

Umoja huo umesema kuwa itaikubali Ukraine, pindi washirika wa NATO watakapokubali na kuona kuwa Ukraine inakidhi vigezo vinavyotakiwa.

Huu ndio ujumbe uliotolewa na muungano wa kijeshi wa Atlantiki katika taarifa yake ya siku ya kwanza kati ya siku mbili za mkutano wao wa kila mwaka huko Vilnius, mji mkuu wa Lithuania.

Hata hivyo Mkurugenzi mkuu NATO, Jens Stoltenberg, aliahidi kuharakisha mchakato wa kujiunga kwa Ukraine.

Pia, alitangaza kuundwa kwa Baraza jipya la NATO-Ukraine, ambalo litafanya mkutano wake wa kwanza siku ya Jumatano na kuipa Kyiv haki ya kuitisha mikutano ya muungano mzima.

Hata hivyo, maendeleo haya hayaonyeshi kwamba NATO itaikubali Ukraine katika muda mfupi kwani haijaonyesha hata tarehe ya kuanza kwa mchakato huo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,