ZINAZOVUMA:

“Chunguzeni mateso na mauaji kwenye hifadhi”

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua...

Share na:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza matukio yote yaliyotolewa taarifa kuhusu kuteswa, kuumizwa na kuuawa kwa baadhi ya Wananchi waliotuhumiwa kuingia ndani ya hifadhi na watakaobainika wachukuliwe hatua stahiki.

Ametoa agizo hilo leo Alhamisi (Aprili 27, 2023) Bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kusimamia masuala ya uhifadhi.

Amesema kuwa Operesheni zote katika maeneo ya hifadhi zifanyike baada ya wananchi wa maeneo husika kushirikishwa na kupewa taarifa za kutosha na sio kuvizia. Kufanya hivyo kutaiwezesha Serikali kuendelea kuimarisha uhifadhi endelevu kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wahifadhi wahakikishe wanazuia mapema wananchi kuanzisha shughuli za kilimo, ufugaji na makazi ndani ya hifadhi. “mkifanya hivi tutaepuka uhitaji wa kuondoa shughuli ambazo zimeshaanzishwa kama vile kuvunja makazi, kufyeka mazao au kukamata mifugo”

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya