ZINAZOVUMA:

Chama cha soka Saudia chazuia usajili wa Mason Greenwood

Chama cha soka nchini Saudi Arabia kimehofia kumsajili mchezaji wa...

Share na:

Chama cha soka nchini Saudi Arabia kimeonyesha hofu ya kuruhusu klabu ya Al Ettifaq ya nchini humo kumsajili mchezaji wa zamani wa Manchester United Mason Greenwood.

Greenwood amepewa mkono wa kwaheri na klabu yake ya Manchester United baada ya kuwa anakabiliwa na mashtaka ya ukatili dhidi ya wanawake.

Al Ettifaq ya Saudi Arabia ilionesha nia ya kutaka kumsajili baada ya kuachwa lakini chama cha soka nchini humo kimesema hakitaki kuharibu taswira yao.

Shutuma zilizokua zikimkabili Mason zimeendelea kumtafuna na kuharibu taaluma yake na huku mashabiki wa kike wa mpira wa miguu wakiwa mstari wa mbele kupinga asipewe nafasi.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya