ZINAZOVUMA:

CCM Zanzibar yamfuta uanachama Karume

Chama cha CCM Zanzibar kimemfuta uanachama kada wake Balozi Ally...

Share na:

Halmshauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja kimemfuta uanachama kada wake Balozi Ali Karume.

Kikao cha kumfuta uanachama Balozi Karume kimefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 8, 2023 chini ya Katibu wa Mkoa wa CCM, Amina Mnacho.

Taarifa ya kumuondosha kwenye chama hicho ilitolewa na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Ali Timamu Haji.

Hatua hiyo inakuja baada ya chama hicho kumpa onyo kutokana na kauli zake akidaiwa kukidhalilisha chama na kuwatukana viongozi wakuu hadharani.

Kutokana na matamshi ambayo Balozi Ali Kalume amekuwa akiyasema likiwemo la kuwa CCM Zanzibar haijawahi kushinda uchaguzi na hujuma za kutwaa ardhi ya familia yao zinazofanywa katika Serikali ya Raisi Mwinyi, kikao cha CCM kilichokaa jana usiku huko Zanzibar kimemfuta uanachama Balozi Karume.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya