Baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF) kubadilisha jina la mashindano yake mapya Super League na kuitwa African Football League
Rais wa CAF Patrice Motsepe amesema mashindano hayo yataanza Octoba 20, 2023 na mchezo wa ufunguzi utachezwa Tanzania.
Timu nane pekee zitashiriki mashindano hayo zikiwemo timu zilizofuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023 Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance ya Tunisia, na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Nyingine zitakazoshiriki ni TP Mazembe ya DR Congo, Enyimba ya Nigeria, Simba ya Tanzania na Petro Atletico ya Angola.