ZINAZOVUMA:

Bwawa la Nyerere kuanza kazi

Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema bwawa la Mwalimu Nyerere...

Share na:

Serikali imetangaza kuwa, wiki moja ijayo kina cha maji katika bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) litakuwa na uwezo wa kuanza kuzalisha umeme.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 31, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka 2023/24 ambayo ameliomba Bunge lipitishe jumla ya Sh3.048 trilioni.

Waziri Makamba amesema kuwa ujazo wa maji uliofikiwa katika Bwawa hilo ni mita za ujazo 163, lakini kiwango kinachotakiwa bado mita za ujazo mbili.

“Mheshimiwa Spika, ninafurahi kulitaarifu Bunge lako kuwa, wiki ijayo hata tukiamua kuanza uzalishaji wa umeme tunaweza kwani kiwango cha chini cha uzalishaji maji tumebakiza mita za ujazo mbili tu,” amesema Makamba.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya