Mfanyabiasha na Bilionea kutoka nchini Kenya Julius Mwale amejitokeza kuwa mmoja wa matajiri wanaowania kununu hisa za jarida maarufu la nchini Marekani la ‘Forbes’.
Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba tajiri huyo yupo tayari kutoa zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 ili aweze kununua hisa kutoka katika jarida la Forbes.
Jarida la Forbes limekua likiaminika kwa zaidi ya miaka 100 sasa likitoa habari za biashara na uchumi duniani kote.
Taarifa zaidi zinasema Mwale ndio anaongoza Kwa kutoa pesa nyingi zaidi miongoni mwa watu waliorodheshwa katika kununua hisa 82% za jarida hilo la Forbes.