ZINAZOVUMA:

Benki ya NCBA kununua kampuni ya Bima ya AIG

Benki ya NCBA nchini Kenya imetangazaa azma ya kununua hisa...

Share na:


Benki ya NCBA-Kenya imeonyesha nia ya kununua hisa za Kampuni ya Bima ya AIG nchini humo.

Benki hiyo imeonyesha nia hiyo, baada ya kumuliki hisa chache, ndani ya AIG kwa miaka takriban 18.

Bw. John Gachora, Mtendaji Mkuu wa NCBA, amesema kuwa wamependezwa na ukuaji wa mapato wa kampuni hiyo.

Kampuni ya AIG Kenya ina wanahisa wawili tu, huku AIG Marekani akimiliki theluthi mbili ya hisa zote.

Huku Kampuni ya AIG-Marekani inatarajia mapato ya takriban dola milioni 13 za Marekani kwa mauzo hayo.

AIG Marekani ilikuwa ni mwanahisa mkuu katika kampuni ya AIG Kenya, na baada ya mauzo NCBA ndio atakuwa mwanahisa mkuu.

Pia kutokana na kulinda maslahi mbalimbali, mpango huo utaendelea ikiwa tu utaidhinishwa na mamlaka za Kenya.

Tayari benki nyingi zimekimbilia kununua au kuanzisha huduma za bima katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hatua hii ya benki hiyo imekuja baada ya kuonekana, hitajio la huduma za bima kwa wateja wake kuongezeka.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya