ZINAZOVUMA:

Barcelona hawana nia na Messi

Klabu ya Barcelona haijatuma ofa yeyote mpaka sasa ya kuhitaji...

Share na:

Nyota wa Argentina na mshindi wa kombe la dunia Lionel Messi anatarajiwa kufanya maamuzi kuhusu wapi atacheza msimu ujao kwani mpaka sasa klabu iliyotarajiwa kutoa ofa juu yake Barcelona hawajafanya hivyo.

Taarifa zinasema kwamba Messi angependa kurejea Barcelona Lakini uongozi wake umesema hawawezi kusubiri tena ofa kutoka kwao ambayo haijawasilishwa mpaka sasa, licha ya ahadi kuwa klabu hiyo ya Catalan ingefanya hivyo kufikia sasa.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwenye umri wa miaka 35 anataka kusalia Ulaya, baada ya kuondoka Paris St-Germain msimu huu wa joto lakini ofa zinazokuja kutoka Ulaya hazimvutii vya kutosha.

Huko Saudi Arabia kuna tetesi kuwa maafisa wa serikali tayari wanashughulikia kuwasili kwake.

Tetesi hizo zinasema kuwa Messi amekubali ofa nono sana kutoka kwa Al-Hilal na wanajiandaa kwa uhamisho huo. Hii ni ofa ya kuvutia zaidi kwa mchezaji huyo mpaka sasa.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,