ZINAZOVUMA:

Auwa nane kwa kufyatua risasi kiholela

Mtu mwenye silaha amewauwa watu saba waliokuwa dukani wakifanya manunuzi...

Share na:

Mtu mwenye silaha amewashambulia kwa risasi na kuwauwa watu wanane waliokuwa wakifanya manunuzi katika moja ya maduka makubwa kaskazini mwa Dallas, Texas nchini Marekani.

Mamia ya watu waliondolewa kutoka katika maduka ya “Allen Premium Outlets” huku watu walioshuhudia wakieleza kuwa mtu huyo alikuwa akiwafyatulia risasi kiholela wapita njia.

Afisa wa polisi aliyekuwa karibu na eneo la tukio alimuua mtu huyo mwenye bunduki baada ya kusikia milio ya risasi. Baadhi ya walioshambuliwa wanaripotiwa kuwa ni watoto.

Takriban watu saba wanatibiwa katika hospitali ya karibu huku watatu kati yao wakiwa mahututi.

Mkuu wa Zimamoto Allen Jonathan Boyd alisema watu saba pamoja na mshambuliaji huyo walitangazwa kufariki katika eneo la tukio na wawili walikufa wakiwa wanapatiwa matibabu hospitali.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,