Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja bila masharti nchini Sudan.
Mgogoro wa kuwania madaraka kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces, RSF, pamoja na vikosi mbali mbali umeripotiwa kusababisha vifo vya watu 50 na wengi kujeruhiwa.
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeitaja hali hiyo kuwa ni “mapigano ya mauaji.” Mapigano hayo yanaendelea kuripotiwa katika mji mkuu wa Khartoum tangu siku ya Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AU baraza hilo linadai Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan na vikosi vya RSF kutafuta suluhisho la amani kwa haraka na mazungumzo ya pamoja kama njia ya kukuza utulivu na kuheshimu matakwa ya watu wa Sudan kwa kurejesha demokrasia, katiba, utawala wa sheria na uhuru.