ZINAZOVUMA:

Andre Onana mrithi wa mikoba ya David De Gea

Manchester United inatarajia kumtambulisha Andre Onana baada ya kukamilisha usajili...

Share na:

Klabu ya Inter Milan imefikia makubaliano na klabu ya Manchester United kumuuza golikipa wake raia wa Cameron Andre Onana kwenda kurithi mikoba ya David De Gea.

Inaelezwa kuwa makubaliano yaliyofikiwa ni kumuuza kwa Pauni Milioni 43 ili kuchukua mikoba ya David De Gea ambaye ameondoka baada ya kudumu kwa miaka 12

Onana pia ameshakubaliana kuhusu mahitaji yake binafsi na Manchester United na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano.

United inatarajiwa kumtangaza kipa huyo leo Jumatatu Julai 17, 2023 ambapo pia uongozi unashughulikia suala la visa ili akajiunge na wenzake walioko ziarani Nchini Marekani.

Onana anaweza kucheza mechi dhidi ya Arsenal, Jumamosi ijayo, pia United inatarajiwa kucheza dhidi ya Real Madrid na Borussia Dortmund.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya