ZINAZOVUMA:

An nahl yawapongeza wanafunzi waliofanya vizuri.

Taasisi ya An nahl imewapongeza wanafunzi waliohitimu kidatu cha nne...

Share na:

Taasisi ya an nahl trust imewapongeza wanafunzi waliohitimu kidatu cha nne mwaka 2022 na kupata matokeo ya daraja la kwanza na daraja la pili.

Katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 18 March katika ukumbi wa Chuo cha Duce zaidi ya wanafunzi 200 wamepongezwa kwa kutunukiwa vyeti na kupewa zawadi mbalimbali ikiwemo vitabu.

Licha ya zawadi walizopatiwa lakini pia wanafunzi walinufaika kwa kupatiwa nasaha ambazo zitawasaidia katika maisha yao ya sasa wakiwa nyumbani kabla ya kuingia katika hatua nyingne za masomo na hata wakiwa tayari wameingia kidato cha tano na sita au vyuo vya kati.

Miongoni mwa wazungumzaji Ndugu Issa Baruti alizungumza juu ya fursa za muhimu ambazo wanaweza kuziendea wakati huu wakiwa bado wanasubiri kuchaguliwa kidato cha tano.

Fursa hizo ni pamoja na kujifunza ufundi stadi, kujifunza lugha mpya na kujifunza matumizi ya kompyuta kwani ujuzi huo utawaongezea thamani huko waendako lakini pia muda wao watautumia vzuri Kwa sasa wakiwa bado wapo katika likizo ndefu.

Tizii Media ilipata nafasi ya kuzungumza na miongoni mwa wanafunzi na wakaelezea namna ambavyo wanaishukuru an nahl trust kwa kuwaandalia hafla hiyo ambayo imewasaidia katika kuwanasihi lakini pia kuwatia hamasa ili waendelee kufanya vizuri zaidi na zaidi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya