ZINAZOVUMA:

Al-Ittihad yaongeza dau kumpata Mo Salah

Klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia imeongeza dau ili kuweza...

Share na:

Ikiwa imebaki siku moja pekee ili dirisha la usajili liweze kufungwa nchini Uingereza klabu ya Al-Ittihad kutoka Saud Arabia wameandaa dau kubwa kwa ajili ya kumpata Mohamed Salah kutoka Liverpool.

Al-Ittihad wameandaa dau la pauni milioni 118 kwa ajili ya Mo Salah licha ya Liverpool kusisitiza kwamba mshambuliaji huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 31 hauzwi.

Hii ni mara ya pili kwa klabu ya Al-Ittihad kuonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ambae kocha wake hataki auzwe.

Kocha Jurgen Klopp amesema kuwa hatojisikia vizuri ikiwa timu hiyo itashawishiwa kukubali ofa ya Al-Ittihad ya Saudia kwa ajili ya Salah na kuamua kumuuza mchezaji huyo.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya