Serikali ya kijeshi nchini Mali yazuia safari za shirika la Air France nchini humo.
Shirika hilo lilisimamisha safari zake kwenda Mali mwezi Agosti siku chache baada ya mapinduzi ya Niger.
Shirika hilo lilitangaza siku ya jumanne kurudikwa safari za Mali, kuanzia ijumaa baada ya kupata ruhusa kutoka Mamlaka ya ndege nchini humo.
Siku ya jumatano serikali ya Mali ilimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga, na kuzuia safari za Air France nchini humo.
Huku moja ya sababu za kuondolewa kwa Mkurugenzi huyo ikiwa, ni kufanya maamuzi makubwa kama hayo bila kushirikisha mamlaka za juu yake.