ZINAZOVUMA:

Tanzania kupokea ndege mpya ya masafa ya kati

Serikali ya Tanzania inatarajia kupokea ndege mpya ya masafa ya...

Share na:

Serikali ya Tanzania inatarajia kupokea ndege mpya ya masafa ya kati aina ya Boeng 737-9 pamoja na ndege mbili ndogo za mafunzo ambazo zitakua chini ya shirika la ndege la Tanzania ATCL.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 2 Oktoba 2023, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ambapo hafla ya mapokezi hayo itafanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere siku ya kesho tarehe 3 Oktoba, 2023.

Prof. Mbarawa amesema ndege hizo ni miongoni mwa ndege nne mpya ambazo Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliingia mkataba na Kampuni ya Boeng ya Marekani, kwa ajili ya utengenezaji Julai 2021.

Ndege hizo ni mbili za abiria za masafa ya kati aina ya Boeng 737-9 yenye uwezo wa kubeba abiria 181 kila moja, ndege moja ya abiria ya masafa marefu ya Boeng 787-8 Dreamliner (abiria 262) na ndegemoja kubwa ya mizigo ya Boeng 767-300 yenye uwezo wa kubeba tani 54.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya