ZINAZOVUMA:

Afrika kusini kujiondoa ICC.

Raisi wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake ina...

Share na:

Raisi wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake ina Mpango wa kujitoa katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya ICC kwa kile kinachoonekana kuwa mahakama hiyo haitendi haki na inafanya unyanyasaji kwa baadhi ya nchi.

Raisi Ramaphosa aliyasema hayo jana jumanne katika mkutano wake na waandishi wa habari ulioandaliwa pamoja na Raisi wa Finland Sauli Niinisto alizuru nchini humo.

Tangazo la Afrika Kusini linakuja wakati shinikizo likianza kuongezeka kwa nchi hiyo kuchukua hatua juu ya hati ya kukamatwa iliyotolewa na ICC dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Afrika Kusini inatazamiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa jumuiya ya kiuchumi inayojulikana kama BRICS – yenye Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini – Julai mwaka huu huku Putin akitarajiwa kuhudhuria.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya