ZINAZOVUMA:

90 wafa maji wakikimbia kipindupindu Msumbiji

Zaidi ya watu 90 wafa maji nchini Msumbiji katika harakati...

Share na:

Zaidi ya watu 90 wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka kaskazini mwa Msumbiji.

Maafisa katika Jimbo la Nampula wamesema watano wameokolewa kati ya watu 130 wanaaminika kuwa ndani ya kivuko hicho.

Mamlaka za nchi hiyo zinasema wasafiri hao walikuwa wakikimbia mlipuko wa kipindupindu, wakitokea Lunga kuelekea kisiwa cha Msumbiji kando kidogo ya pwani ya Nampula.

Kwa mujibu vyombo Vya habari nchini humo vinasema kivuko hicho kilikuwa na uwezo wa kubeba watu 100 lakini wakati kinazama kilikuwa kimebeba watu wapatao 130.

Shirika la habari la AIM liliripoti kuwa chombo hicho kilipigwa na dhoruba kali wakati kikiwa katikati ya mkondo wa bahari.

Shirika la watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) linasema Msumbiji hivi Sasa inakabiliwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu ambao haujawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya robo Karne.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya