ZINAZOVUMA:

63 wapoteza maisha kwa moto Johannesburg

Zaidi ya watu 63 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia...

Share na:

Zaidi ya watu 63 wamepoteza maisha na zaidi ya 40 wakijeruhiwa kufuatia moto kwenye ghorofa kubwa la makazi mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Msemaji wa huduma za dharura mjini Johannesburg Robert Mulaudzi amesema moto huo umetokea Leo asubuhi na kuteketeza jengo hilo lililoko katikati mwa jiji la kibiashara, huku idadi ya waliofariki ikiendelea kuongezeka.

Bado hatua za uokoaji zinaendelea huku wengi ya waliopoteza maisha ni watu wazima na watoto wachache wakati huo majeruhi wakiwahishwa katika vituo vya Afya.

Mulaudzi amesema kuwa jengo hilo lilikuwa ni makazi yasiyo rasmi ambapo watu wasio na makazi wamehamia kutafuta makao bila makubaliano yoyote rasmi ya kukodisha.

Amesema hilo limefanya zoezi kuwa gumu kwa waokoaji kupekua jengo hilo, hata hivyo chanzo cha moto hakijajulikana mpaka sasa.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya