Zaidi ya watu 26 wamefariki nchini India siku ya Jana Agosti 23, 2023 baada ya daraja lililokuwa likiendelea kujengwa kuporomoka na kuuwa wafanyakazi waliokuwa wakiendelea na ujenzi.
Shirika la SkyNews limeandika kwamba daraja hilo lilikuwa la reli ambalo lilikuwa likijengwa katika mji wa Sairang, jimbo la Mizoram.
Kulingana na mamlaka, shughuli za uokoaji zinaendelea huku watu wengine zaidi wakihofiwa kunaswa chini ya vifusi.
Video na picha zilizochapishwa kwenye mitandao zinaonyesha daraja hilo likiwa limevunjika huku kukiwa na vumbi.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi, ambaye yuko Afrika Kusini kwenye mkutano wa kilele wa makundi ya kiuchumi ya BRICS ametoa salamu zake za pole kwa waliofariki katika tukio hilo.