ZINAZOVUMA:

14 wafariki katika ajali ya Lori mkoani Mbeya

Lori lasababisha ajali mbeya na kuua watu 14 akiwemo mtoto...

Share na:

Takriban watu 14 wamepoteza maisha na wengine 17 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali ya Lori kugongana na magari matatu iliyotokea mkoani Mbeya siku ya Jumatano.

Ajali hiyo ya Lori imehusisha imehusisha Lori na magari madogo matatu ikiwemo daladala ya abiria.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, alisema kuwa janga hilo lilitokea katika eneo lenye mteremo mkali kwenye Milima ya Mbembela majira ya saa saba mchana..

Na inasemekana dereva wa lori alipoteza udhibiti wa gari, na ndipo alipogonga basi dogo, gari la kawaida, na pikipiki kadhaa.

Gari hilo lilikuwa limebeba mawe na linaelekea Mbeya kutoka Dar es Salaam, huku basi dogo lilikuwa likisafiri kutoka Tunduma kwenye mpaka wa Tanzania-Zambia kwenda Mbeya.


“Walioathirika wote walikuwa abiria katika basi dogo,” Alisema Mkuu wa Mkoa Homera akiliambia shirika la Habari la Xinhua kwa simu.

Akaongeza kuwa majeruhi wengi walikuwa na hali mbaya, walikimbizwa hospitali ya rufaa ya Mbeya.

Homera alisema kuwa katika waliokufa kuan wanaume wanane, akiwemo mvulana mmoja wa miaka minne.

Chanzo – Xinhua

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya