Zaidi ya wahamiaji 10 wamepoteza maisha kutoka katika nchi za ukanda wa jangwa la Sahara baada ya boti waliokuwa wakitumia kuingia Ulaya kuzama katika bahari ya mediteraniani upande wa pwani ya Tunisia.
Raia hao walikuwa wanataka kuingia Ulaya kwa kunitumia njia isiyokuwa rasmi na ndipo kukutwa na dhoruba hiyo siku ya jumanne ya tarehe 11 Aprili 2023.
Msemaji wa jeshi la ulinzi la Tunisia Houssem Jibabli amesema walifanikiwa kuwaokoa wahamiaji wengine 72 ambao waligundua wanatoka katika nchi za ukanda wa jangwa la Sahara japo hakutaja nchi gani.