Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameyaelezea maisha ya Bernard Kamillius Membe aliyefariki dunia asubuhi ya Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.
Zitto amemwelezea Membe leo Jumapili Mei 14, 2023 katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa siasa, kidiplomasia, wananchi na Serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.
” Membe ulipambana kulinda heshima yako dhidi ya watu waoga ambao badala ya kukukabili kwa hoja waliamua kutuma mtu kukuchafua wewe pamoja na wote tuliokuwa na mawazo mbadala kwa lengo la kutunyamazisha.Kesi yako kupinga kuchafuliwa ulitusemea na sisi sote.”
“Mpaka umauti unakufika Benard Membe hukuacha kulionesha taifa na dunia namna tunapaswa kuhusiana hata kama tunapingana kimawazo na kimirengo ya kisiasa.” Miongoni mwa maneno aliyoyaongea Zitto Kabwe akimuelezea Benard Membe.
Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alijiunga na ACT Wazalendo Julai 15, 2020 kisha kurejea CCM Mei 29, 2022.