ZINAZOVUMA:

ZIMBABWE yaondoa kodi kwenye mbolea

Kutokana na tishio la El Nino Zimbabwe imeondoa kodi ya...
Watu wakipanga mbolea katika ghala

Share na:

Kutokana na tishio la mvua za El Nino, Zimbabwe imefuta kodi ya mbolea kutoka nje.

Lengo la kufuta kodi hiyo ni kuruhusu watu waweze kuinunua kwa wingi, na kuongeza uzalishaji mashambani.

Hatua hii ya Zimbabwe imekuja baada ya shirika la chakula duniani (FAO), kutoa tahadhari ya ukosefu wa chakula kutokana na mvua hizo.

Gharama za mbolea nchini Zimbabwe zilipanda kwa asilimia takriban 30 miaka miwili iliyopita, kutokana na ongezeko la bei ya gesi pamoja na vita vya Urusi na Ukraine.

Gesi asilia “Natural Gas” ni moja ya malighafi inayotumika kuzalisha mbolea za viwandani, na kupanda kwa gharama zake kunaathiri moja kwa moja bei ya mbolea.

Katika kukazia hatua yake hiyo, nchi hiyo inatarajia kuingiza takriban tani laki mbili na nusu za Urea na Ammonium Nitreti bila kodi.

Tangazo lililotolewa na serikali ya Zimbabwe limeondoa kodi hiyo kwa miezi kumi na mbili, kwa waagizaji walioruhusiwa na serikali.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,