ZINAZOVUMA:

MNADA wa vitalu vya gesi mwakani

Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli nchini...
Waziri wa Nishati Mhe. Biteko akizungumza na watumishi wa Pura. Kushoto kake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pura Eng. Charles Sangweni.

Share na:

Mamlaka ya udhibiti wa Mkondo wa juu wa Petroli (PURA) nchini Tanznaia, inatarajia kupiga mnada vitalu vya gesi mapema mwakani.

Mamlaka hiyo inauza vitalu hivyo ili kuongeza Kasi katika utafiti wa mafuta na gesi nchini.

Hii itakuwa ni raudni ya 5 ya uuzwaji wa vitalu hivyo, na inatarajiwa kufanyia robo ya kwanza ya mwaka ujao.

Wanunuzi wakubwa wanatarajiwa kutoka bara ulaya, kutokana na Urusi kuwekewa vikwazo mbalimbali katika upande wa nishati duniani.

“Tnatarajia kufungua mnada huo tukiwa na vitalu 26, na sio vyote” alisema Bw. Charles Nyange, mkuu wa idara ya Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Maudhui na Wadau.

Na kuongeza kuwa ni vyema kutoweka vitalu vyote katika mnada mmoja, bali kuvitenganisha vikawa katika minada ya muda tofauti.

Katika vitalu hivyo vitakavyouzwa, vipo vya majini na nchi kavu.
na kuongeza kuwa hakutakuwa na haja ya kununua zabuni na taarifa za utafiti wa, bali mifumo ya kidijitali itatumika.

“Wataalamu kwa sasa wanaweka mipaka ya vitalu, na wakimaliza mnada utafanyika” alisema bwana Nyange.

Mcahakato huo wa kuandaa taarifa hadi kufikia hatua yam nada wa vitalu hivyo, unatarajia kugharimu serikali takriban Bilioni 3.5.

Na katika kufanikisha zoezi hilo, tayari mwaka huu imetengwa milioni 500 kwa kazi hiyo.

Mnada ni Juni 2024

Mamlaka ya mkondo wa juu wa petroli nchini Tanzania, imesema rasmi kuwa inatarajia kuuza vitalu vya gesi asilia kwa mnada mwezi juni mwaka 2024.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa PURA Mha. Charles Sangweni, katika maonyesho ya Mafuta na gesi ya Afrika, Cape Town – Afrika Kusini.

Mhandisi Sangweni amesema kuwa wanatarajia kukamilisha mauzi ya leseni hizo mwezi Disemba 2024, na kukabidhi leseni kwa walioshinda zabuni hizo.

Na kuongeza kuwa wanatarajia kuuza vitalu 26, ila idadi hiyo inaweza kubadilika hapo baadae.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya