ZINAZOVUMA:

Sekta ya madini kipaumbele cha bajeti – Biteko

Waziri wa Madini Mhe Dotto Biteko amesema kuwa serikali itahakikisha...

Share na:

Waziri wa Madini Dotto Biteko, amesema Serikali itahakikisha inaondoa vikwazo vyote kwa wawekezaji sekta ya madini, hasa kwa kampuni zinazochangia zaidi ya asilimia 60 ya mapato kwa sekta hiyo ikiwamo ya uzalishaji wa madini ya kimkakati.

Akizungumza katika kikao cha jukwaa la majadiliano kati ya wizara na wawekezaji wakubwa kwenye sekta hiyo, Waziri Biteko amekiri uwepo wa changamoto kadhaa ambazo serikali kupitia bajeti ya mwaka huu wa fedha, watazishughulikia.

“Ni kweli kumekuwa na changamoto za kikodi na usimamizi, lakini kupitia bajeti hii iliyoanza Julai Mosi, kuna maeneo mengi yameshughulikiwa,” amesema Biteko.

Jukwaa hilo ambalo linajulikana kama ‘Mining breakfast Briefing,’ lilianza rasmi katika robo ya kwanza mwaka huu kwa ushiriki wa kampuni zenye leseni kubwa (SML) kabla ya kukutana jana katika mkutano wa robo ya pili chini ya mwamvuli wa Chemba ya Madini Tanzania (TCME).

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya