ZINAZOVUMA:

WHO yatoa tahadhari dawa ya kifua ‘Naturcold’

Shirika la Afya duniani limetoa tahadhari juu ya uwepo wa...

Share na:

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari kuhusu dawa ya kikohozi ya ‘Naturcold’, inayosemekana kuwa sio salama kwa binadamu baada ya kuonekana kutumika huko Cameron.

Shirika hilo limesema kuwa viambato vitatu vilitumika kutengeneza dawa hiyo ya maji, ambayo ni hutumika kupunguza dalili za homa ya kawaida, mafua na mzio (allergy) ya pua.

Hata hivyo, uchambuzi wa sampuli za dawa ya Naturcold uligundua kuwa, bidhaa hiyo ilikuwa na kiasi kisichokubalika cha ‘Diethylene Gylcol’ ambayo hutumika kama mbadala wa Gliserini.

Kiasi cha 28.6 % kilichotumika ni mara 286 zaidi ya kiwango cha kawaida kinachokubalika kutumika kiligunduliwa kikiwemo kwenye dawa hiyo.

Kikomo cha kawaida kinachokubalika ni sio zaidi ya 0.10% ‘Diethylene Gylcol‘,
Mchanganyiko huu unapotumiwa kinyume na utaratibu huwa sumu kwa binadamu na inaweza kusababisha kifo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya